May 5, 2015

KAZIMOTO
Timu ya Al Markhiya ya imekumbana na kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Al Rayyan katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Al Markhiya ndiyo timu anayoichezea Mtanzania Mwinyi Kazimoto, ilikumbana na kipigo hicho katika Ligi ya Qatar ikiwa ugenini.

Pamoja na kipigo hiyo, Al Markhiya inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31.

Al Mesaimeer inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 44 ikifuatiwa na Al Mu’aidar yenye pointi 40.

Kipigo hicho kutoka kwa timu isiyo top 5, kimeifanya Al Markhiya kuzidi kupoteza nguvu angalau ya kuwania ubingwa.

 Takwimu zinaonyesha Al Markhiya,  imecheza mechi 17, kati ya hizo 8 nyumbani na 9 ugenini. Imeshinda 9, kati ya hizo 7 nyumbani na 2 ugenini.

Sare ni nne, moja imetoka ikiwa nyumbani na tatu ikiwa inacheza ugenini.


Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 37, lakini safu ya ulinzi imeonekana kutokuwa imara kwa kuruhusu mabao 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic