May 20, 2015


Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema haupo tayari kumuuza kipa wake Said Mohammed kwenye kikosi cha Azam FC.


Hivi karibuni iliripotiwa kuwa kipa huyo anaweza kwenda Azam kwa mshahara wa Sh milioni mbili kwa mwezi na dau la usajili milioni 30.

Kipa huyo amekuwa akihusishwa kuwa huenda akatua katika Klabu ya Azam FC na ikishindikana timu yake ya zamani ya Yanga.

Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema kuwa kipa huyo ni mali yao na haendi popote, ataendelea kuitumikia  timu hiyo huku wakimkaribisha nyumbani aliyekuwa kipa wa timu hiyo, Hussein Sharifu ‘Cassilas’.

 “Said Mohamed atabaki kuwa mali yetu na haendi popote, kwa sasa tumembadilisha kwa kiasi kikubwa na wengine sasa ndiyo wameanza kumtolea macho, ataendelea kuitumikia timu yake kama kawaida, hayo yanayoendelea sasa ni maneno tu.

“Na tumekuwa na kawaida ya kutengeneza makipa bora kutokana na uwezo wa kocha wetu ambaye hata timu ya taifa imemuamini na kuweza kumpa majukumu.

“Vilevile tunamkaribisha Casillas nyumbani kama huko aliko anaona mambo hayaendi sawa, hapa ni nyumbani na aliondoka kwa amani na tulimruhusu sisi wenyewe, hivyo anakaribishwa,” alisema Kifaru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic