May 27, 2015


Siku chache baada ya aliyekuwa winga wa Mbeya City, Deus Kaseke kusajiliwa na Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amefunguka kuwa, anafurahi kumpata mchezaji huyo kwa kuwa aliacha mapendekezo asajiliwe.


Winga huyo amepewa mkataba wa miaka miwili mara tu baada ya kumaliza mkataba na timu ya awali ambayo ameitumikia kwenye ligi kuu kwa misimu miwili tangu ilipopanda daraja 2013/14.

 Akizungumza kutoka nchini Ghana, kocha huyo alisema kuwa kwa sasa yupo mapumzikoni na familia yake lakini anafurahi kwa kuwa alichopendekeza kimefanyiwa kazi.

Kocha huyo aliyeipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema kuwa atarejea mapema nchini na hapo ndipo atapata nafasi ya kuzungumzia zaidi masuala ya usajili.

“Siwezi kuzungumza sana, kwa sasa niko mapumzikoni lakini ukweli ni kwamba alikuwa ni mmoja wa wachezaji niliokuwa nawahitaji kwenye kikosi changu na nilimpendekeza katika ripoti yangu, mengi zaidi tutazungumza nitakaporejea nchini mwezi Juni,” alisema Pluijm.


Winga huyo mwenye kasi na aliyefanikiwa kuichezea Mbeya City kwa mafanikio makubwa licha ya msimu uliomalizika timu yake kuonekana kusuasua, aliziingiza vitani klabu za Simba na Yanga zote zikiwania saini yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic