MAVUGO (KUSHOTO) |
Simba imeamua kumsubiri
mshambuliaji Laudit Mavugo amalize mechi mbili katika kikosi chake cha Vital’O
kabla ya kuja kujiunga nayo kwa ajili ya majaribio.
Lakini vurugu za
kumpinga Rais Pierre Nkurunziza ambaye anataka kugombea kwa muhula wa tatu,
ndizo zimechangia zaidi Simba kufanikisha jambo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye amekuwa akilifuatilia suala hilo
kwa karibu, amekiri vurugu hizo zimechangia kuongeza ugumu wa jambo hilo.
“Kweli hapa kuna suala la
kusubiri amalize ligi na zimebaki mechi mbili. Tumefanya mazungumzo na klabu
yake, pia imani yangu mambo yatakwenda vizuri.
“Lakini mambo mengine
yamekuwa yakikwamishwa na vurugu zinazoendelea Burundi,” alisema Hans Poppe
ambaye ndiye ‘Jembe’ la usajili la Simba.
Mavugo amekuwa tegemeo
katika safu ya ushambuliaji wa Vital’O na aliwahi kufanya kazi na Kocha Goran
Kopunovic.
Kopunovic ndiye
aliyempendekeza Mavugo kwa kuwa alikuwa mchezaji wake akiwa Polisi Rwanda.
Lakini mwisho yeye ameondoka baada ya kutaka apewe dau la Sh milioni 100 ili
asaini mkataba mpya, jambo ambalo Simba hawakukubaliana naye.
Simba imekuwa haina straika
wa uhakika wa ‘kucheka’ na nyavu mara baada ya kumruhusu Amissi Tambwe aondoke.
Tambwe aliondoka Simba
akiwa mchezaji huru, Yanga ikaokota ‘dodo’ na sasa ni kati ya wachezaji
inaowategemea katika ufungaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment