May 5, 2015


Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa kike kutoka Tanzania kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake U-20 mwaka 2016 kati ya Congo DR dhidi ya Gabon.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa jumamosi tarehe 09.05.2015 jijini  Kinshasa, DR Congo, mwamuzi wa kati ni Jonesia Rukya, akisaidiwa na washika vibendera Dalila Jafari na Sophia Mtongoli huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma.

Wakati huo huo Elizabeth Kalinga ameteuliwa kuwa kamisaa wa mchezo kati ya Kenya dhidi ya Botswana kuwania kufuzu kwa michuani ya Olympiki, mchezo utakaofanyika Mei 31, 2015 nchini Kenya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic