June 27, 2015


 Suala la utata wa mkataba kati ya klabu ya Simba na kiungo wake Ramadhani Singano linaonekana kuwa gumu.
Kwani pamoja na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukaa leo, lakini bado jibu halijapatikana!


Sasa suala hilo litawakutanisha tena wiki ijayo kwa ajili ya kujua kipi hasa ni sahihi na kipi ni kosa.

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki amesema kuwa mambo yamekwenda vizuri lakini watakutana tena wiki ijayo.
“Tumekaa kweli, lakini bado naweza kusema kuna mambo kadhaa ya kujadili na mwenyekiti wa kamati amesema tukutane wiki ijayo,” alisema.

Kisoki alikataa kuelezea walipofikia na kusisitiza ni kazi ya mwenyekiti wa kamati huyo ambaye ilikuwa mbinde kumpata.
Tofauti kati ya Singano maarufu kama Messi na Simba ilianza baada ya kiungo huyo kusema mkataba wake unaisha mwaka huu na ulikuwa wa miaka miwili.

Lakini Simba walisisitiza, mkataba huo unaisha mwakani kwa kuwa ulikuwa wa miaka mitatu.

Hata hivyo, TFF ilikubali kusuluhisha, lakini pande hizo mbili huku Messi akisimamiwa na Sputanza, likavurugika zaidi na Simba ikasisitiza lipelekwe kwenye kamati ili kupata mwafaka.

Kushindwa kupatikana kwa mwafaka leo, inaonyesha kuna jambo ambalo linaongeza ugumu na vema likajulikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic