June 30, 2015

HANS POPPE
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe hatimaye amefunguka na kueleza ukweli kwamba wako katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza.



Kiiza raia wa Uganda alikaririwa na gazeti la Championi akisema yuko katika hatua za mwisho kutua Simba.
KIIZA

Lakini jana, Manara alisikika akihojiwa na EFM na kusema si habari za kweli akisisitiza Simba watatoa habari sahihi.

Kauli hiyo ya Hans Poppe inaonyesha kuwa Manara hakuwa akijua kwamba Simba iko katika harakati za kumsajili Kiiza ambaye sasa yuko kwao nchini Uganda.

"Kweli tuko katika hatua za mwisho, kuna watu walikuwa wanashughulikia suala hilo. Nikikutana nao nitajua nini kinaendelea.

"Lakini kama tukifanikiwa kumpata Kiiza, tunaamini atatusaidia. Nafikiri tukishakuwa tumemaliza, basi tutawataarifu," alisema Hans Poppe.

Kiiza alikuwa mmoja wa wafungaji tegemeo wa Yanga kabla ya kutemwa baada ya Kocha Marcio Maximo kuonyesha kutovutiwa naye.


2 COMMENTS:

  1. Manara alikuwa sahihi kutotangaza habari ambazo hazijawa official!! Huyo Hans hajui ethics za kiutawala na kama haoni sababu za kuwa na msemaji wa club ni bora wamfukuze kazi. Huwezi kuwa na taasisi amabayo kila mmoja anatoa taarifa tena un-officially!! Hiyo inafanyika bar tu

    ReplyDelete
  2. Kiukweli Manara yuko sahihi tatizo la Poppe ni kuingilia kazi ya msemaji tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic