June 30, 2015



 
Mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Millard Ayo leo alifanya ziara fupi katika gazeti maarufu la michezo la Championi.


Millard alifanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Mhariri Kiongozi wa Championi, Saleh Ally “Jembe”.
 
Mtangazaji huyo alipata nafasi ya kuelezewa namna unavyokuwa uandaaji ya gazeti hilo la michezo hadi utengenezaji.

Baada ya hapo alibadilishana mawazo na waandishi pamoja na wahariri wa gazeti hilo kabla ya kutembelea sehemu nyingine za Global Publishers pamoja na magazeti yake.
 
Millard ni kati ya wadau wa michezo na amekuwa akijipatia mashabiki na wasikilizaji wengi wa kipindi chake kutokana na umakini wake, pia tabia yake ya kujituma.

Mtangazaji huyo ambaye pia ni mdau wa michezo na amekuwa akitupia stori za michezo kupitia mtandao wake wa www.millardayo.com, amesema amejifunza mambo mengi katika ziara yake hiyo fupi.













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic