July 1, 2015



Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dokta, Joel Bendera ameipongezs TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13),  na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.


Bendera amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio pia amepongeza juhudi za Chama cha Soka mkoa wa Manyara na TFF kwa kuandaa kozi za makocha na waamuzi, akisema huo ndiyo uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya soka mkoani Manyara.

Aidha aliwaasa makocha kutumia mbinu za kisasa za ufundishaji soka walizozipata kwenda kuendeleza vipaji vya wachezaji watakaowafundisha.

Pia Bendera amewahakikishia wakazi wa Manyara atahakikisha wanaandaa vipaji vitakvyowawezesha kuwa na timu bora itakayowakilisha mkoa wa Manyara.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic