July 6, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema hataelekeza nguvu zake sasa katika ushindani wa kikosi chake dhidi ya Azam FC na Yanga.


Kerr raia wa Uingereza amesema hatafanya hivyo ili kuepuka kupoteza umakini wa kukiandaa kikosi chake.
Ameshapewa taarifa za upinzani dhidi ya timu hizo, lakini anaamini ligi ni ushindani wa timu zote.

 “Nilishaambiwa na hata mimi mwenyewe nimefuatilia kwamba hapa Yanga na Azam ndiyo wapinzani wakubwa wa Simba na hata mechi zao huwa ngumu sana lakini sihitaji kuliangalia hilo sana zaidi ya kutazama hizi nyingine 13 zilizobaki ambazo naamini ndizo zenye faida zaidi kama tutafanikiwa kuwa na matokeo mazuri,” alisema Kerr.

Tayari Kerr ameanza maandalizi ya kukinoa kikosi chake mara baada ya kuingia kandarasi ya kuinoa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic