July 29, 2015

 
MISHETTO (WA KWANZA KUSHOTO WALIOPIGA GOTI AKIWA NA KIKOSI CHA RABESTEIN FC.
Kiungo wa zamani wa Stand United ya Shinyanga, Charles Mishetto ametoa pasi mbili za bao 'asisti' katika mechi ya kirafiki akiichezea timu yake nchini Ujerumani.


Misetto amesema walikuwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya ligi kuanza. Mishetto anakipiga katika kikosi cha Rabestein FC kinachoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani.

“Ligi inaanza Agosti 8, hivyo tuko katika maandalizi ya mwisho na tunapambana kweli.


“Ilikuwa mechi nzuri na tumeshinda mabao matatu. Nilicheza dakika zote tisini. Kocha alinipanga namba sana, nikatoa krosi mbili za mabao,” alisema Mishetto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic