July 6, 2015


Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu sasa ameamua kufanya mazoezi ya ziada ili kukabiliana na ushindani mkubwa wa namba.


Busungu anayemudu kucheza namba tisa na 10, kwa sasa anapata changamoto kubwa kutoka kwa washambuliaji wazoefu wa kimataifa wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Kutokana na hali hiyo, Busungu ameamua kujifua vilivyo ili aweze kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kama ilivyo kwa kiungo wa timu hiyo Salum Telela ambaye anaweza kucheza kwa ufanisi nafasi tano.

Busungu amesema kuwa anatamani zaidi kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wakiunda kikosi cha kwanza cha timu hiyo lakini kutokana na ushindani wa namba uliopo katika kikosi hicho, imembidi afikie uamuzi huo.

“Huu ndiyo wakati wangu wa kupambana kwa sababu bado nina nguvu, nikizembea nitashidwa kutimiza ndoto zangu.

“Ili niweze kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, inabidi niwe na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi nyingi uwanjani na sasa najifua vilivyo ili niweze kutimiza lengo langu hilo, nafanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi nakuwa na timu na jioni nakuwa mwenyewe Coco Beach,” alisema Busungu ambaye alisajiliwa na Yanga kwa kitita cha Sh milioni 25 akitokea Mgambo JKT ya Tanga.


“Nikiendekeza uvivu sitaweza kucheza kabisa mbele ya akina Tambwe, Ngoma na Sherman ambao wamekuwa wakiniumiza kichwa kwelikweli.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic