July 6, 2015



Simba iko katika hatua za mwisho za kumalizana na mshambuliaji raia wa Brazil ambaye atafanya kazi ya upachikaji mabao kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Okwi ambaye imemuuza nchini Denmark.

Simba imemuuza Okwi katika klabu ya Sonderjyske ya nchini Denmark.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema raia huyo wa Brazil aliwahi kucheza soka katika Falme za Kiarabu (UAE) na kuwa mmoja wa washambuliaji nyota.

“Tunajua Okwi anaondoka, hivyo ilikuwa ni lazima kusaka wachezaji wenye uwezo wa juu zaidi ili kuboresha safu yetu ya ushambuliaji.

"Kuna Mavugo kutoka Burundi, halafu Mbrazili anayekuja hivi karibuni.


“Huyo Mbrazil ni mmoja wa washambuliaji bora kabisa, tuko katika hatua za mwisho naye atakuja mara moja kuanza kazi,” alisema Hans Poppe ambaye ni jembe la usajili Simba.

1 COMMENTS:

  1. Mmmmmmh! Mshambuliaji bora kabisa anacheza falume za kiarabu!? Tuache siasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic