July 31, 2015


Pamoja na kufanikiwa kucheza vizuri sana katika michuano ya Kagame, beki Serge Wawa wa Azam FC amesema kama mchezaji hayuko fiti katika michuano ya Kagame, anaweza ‘kufa’.


Wawa alisema ‘kufa’ akimaanisha mchezaji hatafanikiwa kuendelea kwa maana ya hataweza.

Akizungumza na SALEHJEMBE mara tu baada ya mechi yao dhidi ya KCCA ambayo wameshinda na kutionga fainali ya michuano hiyo, Wawa raia wa Ivory Coast amesema mechi zimekuwa zikichezwa haraka haraka kwa maana ya karibu karibu.

“Unapumzika siku moja tu baada ya kucheza mechi ngumu kama ile dhidi ya Yanga, unarudi tena uwanjani kucheza.

“Baada ya mechi ngumu kama ya leo dhidi ya KCCA, tunakwenda kwenye fainali baada ya kupumzika mechi moja tu.

“Tunakutana na Gor Mahia, nao wako vizuri sana. Hivyo ni ushindani tena mgumu sana,” alisema Wawa.


Wawa ameingoza safu ya ulinzi ya Azam FC kutofungwa hata bao moja hadi sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic