August 2, 2015



Azam FC imeingia fainali ya Kombe la Kagame, inakipiga na Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Ni fainali ya pili ya Azam FC ndani ya miaka mitatu tu. Lakini inasubiri rekodi ya aina yake kwa kuwa hadi inafika hapo, haijafungwa hata bao moja katika michuano ya mwaka huu.

Hata kama itafungwa bao moja au mawili leo, itaondoka na rekodi ya kuwa na difensi bora kabisa.

Lakini ikibeba kombe bila kufungwa, basi itakuwa imeweka rekodi ya kuwa bingwa wa aina yake mwenye safu ya ulinzi ya chuma.

Kwa Watanzania, furaha ni kuona Azam FC inatwaa kombe na kulibakiza nyumbani.


KILA LA KHERI AZAM FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic