August 3, 2015

SHERMAN AKIWA KATIKA SARE YA MPUMALANGA BLACK ACES MARA TU BAADA YA KUSAINI MKATABA LEO ASUBUHI.
Kpah Sherman amekamilisha usajili wa miaka mitatu katika klabu ya Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini.


Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga raia wa Liberia aliyezaliwa miaka 23 iliyopita tayari anaonekana akiwa katika mtandao wa timu hiyo ukithibitisha kujiunga na klabu yao.

Taarifa zinaeleza ameuzwa dola 150,000, hata hivyo zimekuwa hazina uhakika kwa kuwa Amazayon na Yanga wameficha kuhusiana na uhamisho huo.

Mwenyekiti wa klabu hiyo maarufu kama Amazayon amejivunia kufanikiwa kumnasa Sherman akimfananisha na George Weah.

Mario Morfou amesema:
“Ni mchezaji mzuri anayeweza kutusaidia katika Ligi ya PSL. Tunaamini atashirikiana vizuri sana na Collins Mbesuma kuhakikisha tunafanya vema.

“Ni mshambuliaji aliyechukua ubingwa katika nchi mbili, bado kidogo amfikie George Weah ambaye ni gwiji wa Liberia, Afrika na dunia nzima ambaye alichukua mara tatu.

Sherman ambaye alijiunga na Yanga  akitokea katika klabu  Centikaya Turk S.K. hakuonekana kuwa msaada mkubwa kama alivyoonyesha awali katika mechi ya kumpima kabla ya kujiunga.


Aliichezea Yanga mechi ya kwanza dhidi ya Simba ikiwa ni siku moja tu baada ya kutua nchini, akaonyesha uwezo mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic