August 1, 2015


Kocha mkongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki, Jacob Ghost Mulee amesema beki wa Azam FC, Serge Wawa kama asingekuwa mwanasoka, basi alipaswa kuwa mwanajeshi.


Mulee ambaye ni raia wa Kenya na mchambuzi katika runinga ya SuperSport ameonyesha kuvutiwa sana na Wawa.
“Utaona anavyoiongoza safu yake ya ulinzi, inaonyesha wazi ni mtu anayeijua kazi yake.

“Si mwoga, akiingia anaingia kweli. Anacheza kama beki mahiri anavyotakiwa.

“Lakini anaweza kusaidia kupandisha mashambulizi ya kikosi chake. Naona kama asingekuwa mwanasoka, basi alipaswa kuwa mwanajeshi,” alisema Mulee.

Wawa ameiongoza safu ya ulinzi ya Azam FC kutofungwa hata bao moja hadi inaingia fainali ya michuano ya Kagame itakayochezwa kesho.


Mechi hiyo kati ya Azam FC na Gor Mahia inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki huku Azam ikiwa haijafungwa hata bao moja na timu hiyo ya Kenya iliyofungwa mabao 6, lakini haijapoteza hata mechi moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic