August 28, 2015


 
NDAYISENGA
Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kuchana na Wasenegali wote na sasa inamrudisha Kelvin Ndayisenga.


Ndayisenga raia wa Burundi alifanya majaribio Simba ana kufuzu lakini ikawa tatizo katika suala la makubaliano kigedha.

Pamoja na kutaka dau la zaidi ya Sh milioni 80, Ndayisenga alitaka alipwe Sh 200,000 kwa kila bao atakalofunga.

Simba ikaamua kuachana naye na kumleta Papa Niang kutoka Senegal ambaye alishindwa kuonyesha uwezo.

Aliposhindwa, ikamshusha Abdoulaye Nd’aw ambaye pia alionyesha hana lolote baada ya kuanguka mazoezini akionekana hayuko fiti.
Taarifa zinaendeleza Ndayisenga anarejea Dar es Salaam kujiunga na Simba baada ya Simba kukubaliana na wakala wake, Denis Kadito, Mtanzania anayeishi nchini Uholanzi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic