August 28, 2015

LIBYA
Na Saleh Ally, Kartepe
Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo Ijumaa kucheza mechi ya mazoezi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Libya ambayo pia imeweka kambi katika mji huu wa Kartepe, Uturuki.


 Taarifa zilizotoka jana usiku, mechi hiyo itapigwa saa 5 asubuhi kwa saa hapa pia nyumbani Tanzania

Libya inanolewa na kocha maarufu na mkongwe duniani, Javier Clemente, raia wa Hispania, ambaye amewahi kuzifundisha klabu maarufu na timu mbalimbali za taifa.
 
CLEMENTE AKISALIMIANA NA GUARDIOLA WAKATI WOTE WAKIZIFUNDISHA BARCELONA NA ATLETICO MADRID. 

Clemente ,65, raia wa Hispania, aliyewahi kuzinoa klabu za Athletic Bilbao, Atletico Madrid, Real Betis, Real Sociedad, Espanyol na Tenerife, amesema ana imani Stars itampa ushindani.

Clemente amesema amefurahishwa kuona Stars ina wachezaji wengi vijana.

“Nilipita tu kwenye mazoezi yao, inaonekana wana wachezaji wengi sana vijana. Ndiyo maana nakuambia nategemea upinzani wa juu.

“Najua Ijumaa kutakuwa na mechi nzuri ya mazoezi na hilo ndilo hasa lengo la kuwa hapa. Kufanya maandalizi bora,” alisema Clemente ambaye pia amewahi kuzinoa timu za taifa za Serbia, Cameroon kabla ya kutua Libya.


Kocha huyo amefundisha zaidi ya timu 10 za Hispania katika La Liga, pia amewahi kuinoa Marseille ya Ufaransa, moja ya timu kubwa nchini humo. Licha ya nchi yake kuwa na vita, Libya imekuwa ukihakikisha timu yake ya soka inazidi kuwa imara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic