August 29, 2015

CLEMENTE AKIWAHIMIZA WACHEZAJI WAKE WAPAMBANE DHIDI YA STARS

Saleh Ally, Kartepe
Kocha wa zamani wa Atletico Madrid ambaye sasa anainoa timu ya taifa ya Libya, Javier Clemente ameshangazwa kusikia kuwa kikosi cha Tanzania hakika mchezaji hata mmoja wa kulipwa.

Libya imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stars katika mechi mazoezi ya kirafiki kwenye Viwanja vya Hoteli ya The Green Park hapa Kartepe, Uturuki.

 Katika mechi hiyo, Stars ilifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri na kuipa Libya wakati mgumu kwa dakika zote za kipindi cha pili.
CLEMENTE AKIWA NA GUARDIOLA...
 “Wote wale hakuna hata mmoja anayecheza nje ya Tanzania! Basi mna wachezaji wengi bora,” alisema Clemente ambaye pia amewahi kuzinoa Villarreal, Athletic Bilbao, Levante.

 “Mimi napenda wachezaji wanaoonyesha vipaji, kazi ya kocha inapungua kwa kuwa wanarahisisha uchezaji. Wachezaji wengi wa timu yenu wana vipaji.

 “Tena naona kiasi hata uchezaji unakuwa kama ule wa Hispania kwa kuwa wengi wana maumbo madogo, si wakubwa sana,” alisema kocha huyo aliyezifundisha zaidi ya timu 9 za La Liga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic