August 28, 2015


Na Saleh Ally, Kartepe
Taifa Stars imepoteza mechi yake ya kirafiki ya mazoezi dhidi ya Libya kwa kufungwa bao 2-1.


Mechi hiyo maalum kwa ajili ya mazoezi ambayo haitambuliki na Fifa wala Caf ilifanyika katika moja ya viwanja vya hoteli ya The Green Park hapa Kartepe, Uturuki ambako Stars imeweka kambi ya kujifua.

Bao la ushindi la Libya lilikuwa ni zawadi kutokana na kosa la kipa Said Mohammed Nduda aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ally Mustapha ‘Barthez’.

Nduda ambaye ndiyo alikuwa ametumia dakika nne tu uwanjani, mpira ulimpontoka mara baada ya kuudaka, wakati anajaribu kutoa pasi, akatoa fupi iliyomfikia fowadi aliyekuwa karibu yake na kufunga kiulauni kwa kuwa mabeki walishapanda wakiamini ameushaudaka.


Libya ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 26 baada ya Libya kufanya shambulizi kali.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko huku Libya wakilazimika kujilinda zaidi mwishoni mwa kipindi cha kwanza.


John Bocco aliisawazishia Stars bao katika dakika ya 58 baada ya Simon Msuva kuangushwa katika eneo la boksi.
Baada ya hapo Stars ilikuwa moto kwa kushambulia mfululizo huku Libya wakijilinda zaidi.



Huku ikionekana kama Stars ingeibuka na ushinda kosa la Nduda liliipa nafasi Libya kupata bao la pili hivyo kuilazimisha karibu timu nzima ya Libya kurudi nyuma na kulinda.

Mara mbili Ibrahim Ajibu aliyeingia kuchukua nafasi ya Said Ndemla, Simon Msuva Rashid Mandawa aliyeingia kuchukua nafasi ya Bocco wangekuwa makini wangeweza kuipatia Stars bao.
Mchezaji mmoja wa Libya alilambwa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika 12. Hiyo ilikuwa ni baada ya kumpiga kiwiko Mudathir Yahya aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi ya Frank Domayo.


Stars iliendelea kutawala kipindi cha pili huku Libya inayefundishwa na kocha gwiji kutoka Hispania, Lazaro Clemente ikitumia muda mwingi kujilinda na kubutua mipira hovyo.


 Katika kipindi cha kwanza, Libya ilitawala dakika 15 za mwanzo lakini Stars ikatawala zote 30 ikishambulia mara 13 dhidi ya mara 4 tu ya Libya.

Kipindi cha pili, Stars ikapeleka mashambulizi 16 langoni mwa Walibya hao ambao walishambulia mara nne kwa mara nyingine, tena safari hii wakijilinda zaidi na kubutua mipira hovyo.
STARS...
Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa alifanya mabadiliko ya wachezaji zaidi ya watano ikiwa ni sehemu ya kukijaribu kikosi chake.

Mkwasa alisema kwa kuwa ilikuwa ni mechi ya mazoezi, ilikuwa ni vizuri kutoa nafasi kwa karibu kila mchezaji.
LIBYA

"Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo, tunachofanya ni kutengeneza timu pia kuangalia wachezaji mmoja mmoja," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic