September 2, 2015


Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amsema anaendelea kufuatilia soka ya Tanzania kwa karibu.


Milovan amesema hajaacha kufuatilia mpira wa Tanzania kwa kuwa ni sehemu anayoipenda.

"Najua mengi yanayoendelea, wakati mwingine nipo kazini Mnyamar au nipo mapumzikoni nyumbani Serbia, napenda kujua Simba inafanya nini imefikia wapi.

"Lakini nimekuwa nikiangalia soka la Tanzania kwa timu nyingine zinafanya nini. Azam FC wamechukua ubingwa, ni hatua kubwa kwa mabadiliko ya soka Tanzania," anaeleza Milovan.

Milovan ni kati ya makocha walioipa Simba mafanikio na kinachofanya mashabiki wa soka wasimsahau ni kuingoza Simba kuitwanga Yanga kwa mabao 5-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic