September 2, 2015

SIKU MWAIKIMBA ALIPOTUA JKT

Gaudence Mwaikimba amefunga bao na kuonyesha kiwango wakati Ruvu JKT ikiifunga Azam FC kwa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Azam Complex, jana usiku.


Mwaikimba ambaye alikuwa mshambuliaji wa Azam FC, alionyesha kiwango ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Azam FC katika mechi hiyo ya jana.

Mwaikimba alifunga bao la kwanza katika dakika ya 10, baada ya shuti la Mussa Said kurudi uwanjani baada ya kuwagonga mabeki wa Azam FC.

Bao la ushindi la JKT lilifungwa na Najim Magulu dakika nne kabla ya mechi mwisha.

VIKOSI:
AZAM FC
Mwadini Ali, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Serge Pascal Wawa, Gardiel Michael, Lacine Diouf/Said Mourad dk47, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Bryson Raphael, Ame Ally, Kipre Tchetche na Ramadhani Singano ‘Messi’/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk60. 

JKT

Tony Kavishe, Napho Zubery, Edward Charles, Cecil Kisimba, Martine Kavila, Hamisi Shengo, Ismail Mohammed/Emanuel Pius dk20, Matheo Daniel/Issa Ngao dk80, Gaudence Mwaikimba, Amour Janja/Najim Magulu dk76 na Mussa Said/Jaffar Kisoky dk80.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic