September 1, 2015

WACHEZAJI WA STARS WAKIWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ATATURK NCHINI UTURUKI
Na Saleh Ally, Istanbul
Kikosi kizima cha Taifa Stars kimeondoka jijini Istambul, Uturuki muda mfupi kurejea nyumbani Tanzania.


Stars imeondoka baada ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Nigeria, mechi itakayochezwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.

Stars ilikuwa imeweka kambi hapa Uturuki kujiandaa na mechi hiyo kambi ambayo ilikuwa katika mji wa Kartepe ulio milimani kabisa.
Kikosi hicho kimepanda ndege ya Turkish leo kuanza safari hiyo ya zaidi ya saa 7 kurejea nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mechi hiyo.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic