September 5, 2015


Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema wanaodhani anakiandaa kikosi chake ili kicheze na Simba wanakosea, kwani anaandaa ‘chama’ litakaloifunga timu yoyote.

Pluijm ambaye kikosi chake sasa kinafanya mazoezi ‘mafichoni’ kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam, ameliambia Championi Jumamosi kuwa; “Siyo Simba tu, najiandaa kuzifunga timu zote za Ligi Kuu Bara.”

Huku akicheka na kuonyesha msisitizo, Pluijm raia wa Uholanzi alisema, mashabiki wengi wa Yanga kila wakikutana naye humuuliza kuhusu mechi na Simba jambo linalomshangaza.

“Unajua nashangaa sana, mashabiki wanaiwaza Simba tu wakidhani mimi naandaa kikosi cha kucheza na timu hiyo tu. Wanakosea, mimi najiandaa na mechi za timu zote za ligi ili tutetee ubingwa wetu.

“Itakuwa haina maana kuifunga Simba tu halafu tupoteze ubingwa, najiandaa kuzifunga timu zote siyo Simba tu,” alisema Pluijm mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika.

Yanga imepangwa kucheza na Simba, Septemba 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic