October 7, 2015


 Kuelekea mchezo  wa Yanga na Azam utakaopigwa mapema Oktoba 17, mwaka huu, tayari timu hizo zimeanza mipango ya kujiandaa, huku Azam FC ikisubiri wachezaji wake warejee kutoka timu za taifa na kwenda kuweka kambi ya muda visiwani Zanzibar.


 Msimu uliopita awali, walitoa sare ya mabao 2-2, wafungaji wakiwa ni Amissi Tambwe na Simon Msuva kwa Yanga huku Azam akifunga Didier Kavumbagu na John Bocco na mara ya pili walipokutana, Azam waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 Kikosi cha Azam kimeanza mazoezi rasmi leo Jumanne katika uwanja wake wa Azam Complex, ingawa asilimia kubwa ya wachezaji wapo katika timu zao za taifa.

 Ofisa habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema kuwa kikosi hicho kilianza mazoezi jana Jumanne, licha ya wachezaji wengi kutokuwepo.

Kiongozi huyo alifunguka kuwa, wana mpango wa kutafuta sehemu ya kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao, kama ni hapa Dar au kwenda Zanzibar lakini itategemea na kocha atakavyoamua.

“Ni kweli mipango ya klabu na kocha wetu ni kuhakikisha tunafanya vyema kwa kila mchezo na mchezo uliopo mbele yetu ni dhidi ya Yanga na kama suala la kuweka kambi litakuwa ni pendekezo la kocha, yeye ndiye ataamua kama ni hapa Dar au sehemu nyingine.


“Kwa sababu walioitwa timu za taifa wapo wa nje pia kama Allan Wanga, ni vyema wakaungana pamoja na kuweza kuanza maandalizi kwa pamoja ili kumrahisishia kazi kocha kutokana na kibarua kilichopo mbele yetu, maana msimu huu hakuna timu ya kuidharau, zote zimejipanga,” alisema Idd.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic