October 13, 2015


Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha (pichani) amesema mechi yao dhidi ya Azam FC wikiendi hii itakuwa ngumu na ya hesabu nyingi.

Dk Tiboroha amesema mechi hiyo inakutanisha timu bora katika Ligi Kuu Bara, hivyo kila upande utakuwa unataka kufanya vema.
"Ni mechi ngumu, mechi ambayo inakutanisha timu bora ambazo kila moja itakuwa inataka kushinda mechi hiyo na kujiwekea uhakika wa kukaa kileleni," alisema.
"Sisi tunaendelea na maandalizi, tunapambana kweli ili kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri zaidi kama ambavyo tumeanza."
Yanga kama ilivyo kwa Azam FC hazijapoteza hata mechi moja ya Ligi Kuu Bara na sasa zinakutana.
Kwa kipindi hiki, katika Ligi Kuu Bara, mechi ya Azam dhidi ya Yanga ndiyo gumzo zaidi.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic