October 13, 2015


Beki Shomari Kapombe aliyekuwa majeruhi ameanza mazoezi na kikosi cha Azam FC kinachojiandaa kuivaa Yanga, wikiendi hii.

Kapombe aliumia akiwa na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars lakini sasa yuko tayari kuivaa Yanga kwa kuwa ameanza mazoezi na wenzake.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd 'Mbunifu' amesema mazoezi yanaendelea vizuri na Kapombe ni kati ya wanaoendelea na mazoezi.
"Kapombe ni kati ya wanaofanya mazoezi, anaendelea vizuri na matumaini yapo ataungana na wenzake kwa ajili ya mechi dhidi ya Yanga," alisema Mbunifu.
Mechi kati ya Yanga dhidi ya Azam FC imeendelea kuwa gumzo kwa kuwa ndiyo timu pekee ambazo hazijafungwa Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic