October 6, 2015


Mmliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi amemwaga mamilioni kwa wachezaji wake baada ya kuiwezesha kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mazembe imetinga fainali baada ya kuing’oa El Merreikh ya Sudan, moja ya timu tajiri barani Afrika.



Katumbi ametoa dola 60,000 (zaidi ya Sh milioni 120) ambazo wamegawana wachezaji 24 wa kikosi chake.

Kati ya wachezaji wa kikosi hicho ni Watanzania wawili, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta ambaye alifunga mabao mawili wakati Mazembe wakiinyoa El Merreik kwa mabao 3-0.

Katika mechi ya kwanza ambayo Mazembe walipoteza ugenini, Ulimwengu alifunga bao moja.


Hivyo kufanya mchango wa Watanzania hao kuwa asilimia mia hadi timu hiyo inatinga fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic