October 10, 2015

N'DAW
Kocha wa Simba, Kocha wa Simba, Dylan Kerr anaamini mshambuliaji Pape N’daw bado ana nafasi ya kufanya vizuri katika kikosi chake lakini viongozi wa Simba wanasema hapana.



Tangu N’daw raia wa Senegal atue Simba, hajaonyesha kiwango cha juu kama wengi walivyotarajia, jambo lililowafanya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kumuona kama mzigo kikosini.

Lakini Kerr raia wa England, anaamini N’daw itafika siku ataonyesha mambo, ingawa hajasema ni lini hasa!
 
N'DAW AKIWA MAZOEZINI NA WACHEZAJI WENZAKE WA SIMBA...
Alisema tangu N’daw ajiunge na klabu hiyo, amekuwa na maendeleo mazuri kila siku, hivyo ana uhakika atakuwa na masaada mkubwa ndani ya Simba katika siku chache zijazo.

“Hivi sasa naangalia jinsi gani nitaanza kumtumia katika kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wake mkubwa anaouonyesha uwanjani tunapokuwa mazoezini.

“Wengi wanamuona kama mzigo lakini ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kwa kupiga mashuti langoni, ujue huyu amekuja kwenye soka la kasi na nguvu nyingi tofauti na alikotoka,” alisema Kerr.

N’daw ambaye amekuwa akiingia katika mechi nyingi za Simba amekuwa haonyeshi kiwango bora, hali ambayo inaonyesha kuwashinda hata mashabiki wa Simba.

Wadau wamekuwa wakihoji mchezaji wa kimataifa kuja kukuza kiwango chake Simba tena kwa kutokea benchi, jambo ambalo linashangaza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic