October 13, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema hawawezi kulala eti kisa kwa kuwa Mbeya City wameondokewa na kocha wao.


Kocha Juma Mwambusi ameondoka Mbeya City na kujiunga Yanga akiwa kocha msaidizi.

Kerr raia wa Uingereza amesema Mwambusi ni sehemu tu ya Mbeya City, lakini timu zaidi ya asilimia 90, bado iko vilevile.
 

“Ameondoka mwanajeshi wao mmoja, kweli ni muhimu. Lakini wao bado wana nafasi pia ya kupambana na kuonyesha wanaweza bila ya kuwa na kocha huo.

“Hii itakuwa mechi ngumu zaidi, tutapambana na kuhakikisha tunashinda,” alisema.

Simba ipo mjini Mbeya kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho jijini Mbeya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic