October 7, 2015




Kiroho safi! Kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho kwa mara ya kwanza amefunguka  kuhusu hatima yake ndani ya Jangwani na kusema kuwa kwa hali ya mambo ilivyo kwa vyovyote itakavyokuwa hawezi kubaki.


Hata hivyo, kiungo huyo amesema yupo tayari kucheza timu yoyote ya ligi Kuu Tanzania Bara ikiwemo Simba.

Nyota huyo pamoja na kukubalika kwa mashabiki na baadhi ya viongozi kutokana na uwezo wake wa kumudu winga ya kushoto na mipira iliyokufa, hata hivyo amekosa nafasi ya kudumu kwa siku za hivi karibuni.


Mbrazili huyo ambaye aliletwa nchini na Marcio Maximo amesema, kuwa kwa maisha anayoishi kwa sasa Jangwani, dhahiri shahiri hawezi kubaki hata kama watataka aendelee.

“Kiukweli siridhishwi na maisha ninayoishi kwa sasa. Hata kama angekuwa mchezaji gani, kwa jinsi ninavyoishi hawezi kuridhika nayo. Siwezi kuongeza mkataba kwa hali ilivyo.


“Lakini nitakuwa tayari kubaki huku iwapo kutakuwa na timu yenye kunihitaji hata kama ni wapinzani wetu Simba, ila kama nitaona kimya naondoka kwenda nyumbani kwetu Brazil,” alisema kiungo huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic