October 4, 2015

MAGULI

Mshambiuliaji Elius Maguli ameibuka shujaa wa kikosi chake cha Stand United baada ya kuifungia bao muhimu la ushindi dhidi ya Mbeya City.

Stand United imeifunga Mbeya City kwa bao 1-0 katika mechi Ligi Kuu Bara iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Maguli alifunga bao hilo kwa kumchambua kipa mkongwe Juma Kaseja ikiwa ni baada ya kupokea pasi safi ya Pastory Athanas katika dakika ya 47.


Hilo ni bao la nne la Maguli katika michezo yao sita ya Ligi Kuu Bara waliyocheza msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic