October 6, 2015


Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Malawi, amesema hawajaja kutembea nchini, badala yake watapambana kuhakikisha wanaishinda Stars.


Kocha Msaidizi wa Malawi ‘The Flames’, Ramadhani Nsanzumo amesema wanajua Stars ina kikosi kizuri, lakini akajivunia zaidi chao.

“Tuna wachezaji nane wanaocheza soka nchini Afrika Kusini pia Msumbuji. Wote tuko nao hapa na wengi ni vijana.

“Lakini tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda na kujiwekea mazingira mazuri,” alisema.

Mechi hiyo ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic