October 10, 2015




Mgombea wa Udiwani jimbo la Mbagala Kuu, Dar es Salaam kupitia CCM, Yusuf Manji kesho amepanga kufanya mkutano wake mkubwa kuzungumza na wakazi wa jiji hilo kubwa nchini.

Manji anatarajia kufanya mkutano huo kwenye Viwanja vya Mbaghala Zakheem ambao utakuwa mkutano wake wa kwanza kutangazwa kwani awali, mikutano mingi katika mitaa ya Mbagala Kuu hakuwa akiitangaza lakini bado ilihudhuriwa na watu wengi sana.


Taarifa kutoka CCM Mbagala zimeeleza, mkutano huo utawajumuisha wanasiasa mbalimbali wa eneo hilo pamoja na maeneo jirani.


“Manji amekuwa akifanya mikutano sehemu mbalimbali katika mitaa ya Mbagala Kuu, mkutano wa Jumapili pale Zakhem ni kwa ajili ya Wanadar es Salaam.

“Tunatarajia kuwa na watu wengi huenda kuliko wale waliokuwa wakijitokeza katika mikutano ya wagombea wa ubunge na hata urais,” alieleza mmoja wa waandaaji wa mkutano huo kutoka CCM eneo la Mbagala.



Maandalizi ya mkutano huo yameishaanza na bado haijajulikana Manji atazungumza hasa jambo gani ingawa itakuwa ni sehemu ya kampeni zake.

Imani kubwa kwa Wanambagala kwa Manji imetokana na namna alivyopata mafanikio kupitia katika kampuni zake za Quality Group Ltd.

Lakini mafanikio makubwa akiwa na Yanga ambayo amefanikiwa kuiondoa katika migogoro na timu yake kuendelea kufanya vizuri.



Kwani tokea achukue kiti cha Uenyekiti wa Yanga, kikosi cha Yanga kimekuwa kikichukua ubingwa au kushika nafasi ya pili huku watani wao Simba wakiwa hawajashika nafasi ya pili au ubingwa kwa zaidi ya misimu mitatu sasa.

Mafanikio hayo kibiashara na uwezo wa kuwaunganisha Yanga, ndiyo umefanya watu wengi wa Mbagala kuwa na imani kubwa na Manji ambaye pia amewashangaza wengi kuamua kuwania udiwani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic