October 10, 2015

MISHETO AKIONYESHA PICHA YAKE KWENYE VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO...

Mtanzania Charles Misheto anayekipiga katika timu ya daraja la nne nchini Ujerumani, ameonyesha namna ambavyo soka nchini humo limepiga hatua.


Misheto amesema katika soka nchini humo, maandalizi au namna wachezaji wa timu za daraja la nne wanavyokaa katika vyumba vina ubora wa juu hata kuliko Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Ninacheza daraja la nne, lakini utaona namna mambo yalivyo na mpangilio bora kabisa,” alisema.


“Wenzetu wamepiga hatua na wanaonyesha nia yao kuhusiana na mchezo wa soka, vifaa ni bora, mpangilio wa mambo, ratiba na mambo mengine kwa kweli yanaonyesha hawa watu wanataka kupata maendeleo,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic