October 5, 2015


Na Saleh Ally
Suala la beki wa Mbeya City, Juma Nyosso limechukua sura mpya baada ya kuzua mjadala barani Ulaya.


Pamoja na kujadiliwa mitandaoni, gazeti la siasa la Sweden la Aftonblandet limeandika katika ukurasa wake wa michezo likimjadili Nyosso ambaye amefungiwa kucheza miaka miwili na kulipa faini ya Sh milioni 2 baada ya kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John Bocco kwa kumtomasa makalio, wiki iliyopita.

Gazeti hilo kupitia ukurasa wake Sportsbladet limelielezea suala hilo la Nyosso kuwa ni sehemu ya mambo ya kushangaza katika soka kwa sababu mbili.

Katika ukurasa huo wa michezo, gazeti hilo lililotoka wiki iliyopita lenye kichwa cha habari “Stangs av I tva ar-for oanstandigt uppforande” yaani afungiwa kucheza soka kwa tabia chafu, lilijichanganya kumuita Nyosso ni beki tegemeo wa Taifa Stars tena likitumia picha akiwa na jezi ya Taifa Stars wakati akiichezea.

Hata hivyo, mjadala wa gazeti hilo ulikuwa ni adhabu ya Nyosso kuonekana ni kubwa sana huku baadhi ya waliojadili wakisisitiza, angefungiwa mechi kadhaa.


Wengine kama ilivyo kwa wadau wa soka nchini, walieleza kwamba Nyosso alistahili kupata adhabu kali kwa kuwa alirudia kufanya tendo hilo, lakini si kufungiwa muda mrefu hivyo.

Suala hilo, limekuwa mjadala hata hapa nchini wengine wakiunga mkono adhabu hiyo ya TFF na wengine wakitaka ipunguzwe, wengine wakisisitiza itumike moja iwe kufungiwa au faini na si zote kwa wakati mmoja.

Kabla ya kumfanyia hivyo Bocco kwa mkono wake wa kushoto, Nyosso aliwahi kufanya hivyo kwa mkono wake wa kushoto kwa Elius Maguli akiwa Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic