October 4, 2015

NGOMA.

Mshambuliaji nyota wa Yanga, Donald Ngoma amesema kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara ina ushindani na ngumu sana.


Hata hivyo, Ngoma raia wa Zimbabwe ameapa kupambana hadi mwisho kuhakikisha anaisaidia timu yake, pia anapata mafanikio zaidi.

“Wakati nakuja nilijua ni ligi yenye ushindani sana, lakini sasa naona ushindani ni zaidi ya vile nilivyofikiria na kila mchezaji anataka timu yake ishinde.

“Ninachofanya ni kuendelea kuzoea mazingira lakini bado ninapambana sana kuhakikisha nafanya vizuri,” alisema Ngoma.


Fowadi huyo wa zamani wa FC Plutnums ya Zimbabwe sasa ni tegemeo la safi ya ulinzi ya Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Mshambuliaji amekuwaje tegemeo la safu ya ulinzi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic