October 6, 2015


Hatimaye Kocha Charles Boniface Mkwasa amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Taifa Stars.


Mkwasa amesaini mkataba wa kuinoa Stars ambao utaisha Machi 31, mwaka huu.

"Kweli nimsaini mkataba, nawashukuru sana TFF kwa kuniamini na kunipa jukumu hili," alisema.

Mkwasa ambaye mkataba wake na Yanga uliokuwa unaisha Desemba mwaka huu, amesema amepanga kuwaanga Yanga rasmi.

Kocha huyo tayari ameiongoza Stars kucheza mechi mbili za mashindano akiwa kocha wa muda na aliiwezesha kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda katika michuano ya Chan.

Mechi ya pili, Mkwasa aliiongoza Taifa Stars kutoka sare ya bila kufunga dhidi ya Nigeria katika mechi ya kuwania kucheza Afcon.

Sasa kesho atakuwa na kibarua cha tatu dhidi ya Malawi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kitakuwa cha kwanza kwake akiwa kocha kamili wa Taifa Stars.

Wiki iliyopita, Blogu hii iliandika makala kuitaka TFF iamue moja kuhusiana na Mkwasa katika suala la kumpa mkataba baada ya kusuasua.

Mkwasa ameichukua Stars baada ya Mholanzi, Mart Nooij kushinda na kuifanya iwe sawa na jahazi linaloyumba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic