October 13, 2015

Unajua Rais Jakaya Kikwete ni mwanamichezo? Kama utataka kumuuliza amwaachaje wanamichezo, jibu lake ni lahis sana.

Atakujibu hivi; "Kidongo Chekundu", unajua kwa nini?

Rais Kikwete amesema hilo ndiyo litakuwa jibu lake kwa wanamichezo nchini kwamba baada ya kusaidia michezo kadiri ya uwezo wake, ameamua kuwaachia zawadi ya kituo maalum cha kukuza vipaji cha Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
"Tarehe 17 mwezi huu, ninakwenda kuzindua hicho kituo pale Kidongo Chekundu," alisema Rais Kikwete wakati wa hafla maalum ya kumtuza kutokana na mchango wake mkubwa katika michezo wakati wa uongozi wake kwa miaka 10.

Rais Kikwete alisema: "Kituo hicho kilikuwa ni kwa ajili ya kuendeleza vipaji na Sunderland ya England tayari wameishaleta kocha kwa ajili ya vijana.

"Kampuni ya Symbion ndiyo niliwaomba wajenge kituo hicho, tumekubaliana nao na sasa mambo yanakamilika. Sunderland wao wanafanya kazi ya kukiendesha ikiwa ni pamoja na kukuza vijana.

"Nilipeleka maombi yangu sehemu hizi mbili, yamepita na hii ndiyo zawadi nitawaachia Watanzania wapenda michezo. Wale si soka tu, kuna uwanja mzuri wa basketball.
"NBA nao wataleta mwalimu ambaye atawanoa vijana, hivyo ni faida kubwa kwa vijana na vipaji vya Watanzania," alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wadau waliojitokeza katika hafla hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic