October 12, 2015


Pamoja na Mzimbabwe wa Yanga, Donald Ngoma kuiteka Bongo kwa mabao yake mfululizo lakini mshambuliaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa, ametamka bila woga kuwa ni vigumu staa huyo kutwaa ufungaji bora mbele ya Mganda, Hamis Kiiza wa Simba.

Ngassa aliwahi kuichezea Yanga na sasa anakipiga na Free State ya Afrika Kusini. Lakini pia aliwahi kukipiga Simba.

Kiiza anaongoza kwa kufunga mabao matano kwenye Ligi Kuu Bara, akifuatiwa na Ngoma, Mrundi, Amissi Tambwe wa Yanga na Elias Maguli wa Stand United waliofunga manne kila mmoja.

Ngasa amesema Ngoma anaweza kuukosa ‘ufalme’ huo msimu huu kutokana na ugeni wa ligi ikiwa ni tofauti na Kiiza na Tambwe ambao wanaielewa kinagaubaga Ligi Kuu Bara, hivyo mbinu zote wanazo mkononi.

“Ngoma bado mgeni tofauti na Kiiza na Tambwe ambao wote wamecheza Simba na Yanga na wanafahamu mazingira yote ya ligi, wanajua zaidi ni mbinu gani watumie lakini uwezo wao wa kufunga kila mtu anaujua kwa hiyo utaona wana vitu vingi vinavyowabeba tofauti na Ngoma.


“Lakini angalia hata spidi yao, Tambwe ameshafunga mabao mawili ndani ya mechi moja, Kiiza tayari ana hat-trick tofauti na Ngoma ambaye bado hajaonyesha hilo, kwa upande wangu Kiiza na Tambwe wana nafasi kubwa zaidi ya Ngoma kutokana na vitu vingi na sababu nyingine nilizokupa,” alisema Ngassa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic