October 13, 2015


Mkurugenzi wa duka la Zizzou Fashion, Athumani Tippo (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo kocha wa Changanyikeni Rangers, Steven Nyenge ndani ya duka hilo lililopo maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam mapema leo.

DUKA la vifaa vya michezo la Zizzou Fashion mapema leo lilijitolea kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya Changanyikeni Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.


Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Zizzou Fashion, Athumani Tippo alisema kwamba, amelazimika kutoa mchango wake kwa timu hiyo kutokana na kuonyesha juhudi, uwezo na kujituma kwa wachezaji wa timu hiyo kwa muda mfupi tangu ilipoanzishwa.

“Niameamua kutoa mchango wangu wa vifaa vya michezo kwa timu hiyo kwani imenishawishi baada ya kuifuatilia kwa muda sasa ambapo nimeziona juhudi za kocha wao, Steven Nyenge na wachezaji wote kwa ujumla wanavyojituma kuhakikisha wanapanda daraja,” alisema Tippo.

Tippo aliwahi kuwa beki na kiungo tegemeo wa Milambo ya Tabora, baadaye Coastal Union ya Tanga wakati Nyenge alikuwa kiungo tegemeo wa Shinyanga Shooting ya Shinyanga na baadaye Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic