November 30, 2015

 

Chelsea na Watford ndiyo klabu mbili zitakazomrudisha mshambuliaji Emmanuel Adebayor nchini England.


Adebayor ameamua kusafiri kwenda England tena wiki ijayo na imeelezwa kuna uhakika atafanya mazungumzo na kati ya klabu hizo mbili, moja wapo anaweza kujiunga nayo kwa ajili ya Ligi Kuu England.

Hiyo ni baada ya wiki kadhaa za kuvunja kwake mkataba na klabu yake ya Tottenham na baada ya hapo aliamua kurejea kwao Togo na kuendelea na maisha.

Lakini sasa, anarejea kwa kuwa karibu dirisha la usajili linafunguliwa.
 

Msimu uliopita aliichezea Spurs mechi 17 na kufunga mabao mawili tu. Mechi yake ya mwisho aliichezea Spurs alipoanza lakini akatolewa wakati walipopata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Man City.

Mechi yake ya mwisho ya mashindano kufunga bao ilikuwa ni Oktoba 2014 wakati Spurs ilipoivaa Newcastle.

Hata hivyo, Adebayor anaendelea kubaki mmoja wa wapachika mabao bora England, kwani anashika nafasi ya 26 kwa ubora wa ufungaji katika ligi hiyo maarufu duniani baada ya kuwa amepachika mabao 96 akiwa na Arsenal, Man City na Tottenham. Pia aliwahi kukipiga Real Madrid ya Hispania.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic