November 26, 2015


Na Saleh Ally
Azam FC ndiyo klabu inayofanya vizuri zaidi katika klabu zote za kizazi cha sasa, hilo halina ubishi tena.
Klabu hiyo imekuwa chachu au changamoto kubwa kwa klabu kongwe kama za Yanga na Simba ambazo mambo yake mengi ni ili mradi.


Yanga na Simba ni wakongwe, lakini mambo yao mengi yamekuwa na konakona, utendaji wao pia umekuwa ni ule uliosimamia enzi bila ya kujali mabadiliko.
Ujio wa Azam FC, ingawa mwanzoni ulionekana si kitu si chochote, lakini baadaye joto lilianza kuzipata Yanga na Simba na mwisho hakukuwa na uwezo wa kuizuia.
Ndani ya misimu mitatu, Azam FC imeweza kushika nafasi ya pili mara mbili na ubingwa mara moja. Wstani bora kabisa ambao ukitoa Simba na Yanga, basi inazidiwa na Mtibwa Sugar pekee iliyowahi kutoa ubingwa wa Bara mara mbili.
MAJEGWA (WA PILI KULIA) AKIWA MAZOEZINI SIMBA.
Wamilikiwa Azam FC wanastahili sifa kubwa kwa kuwa wamekuwa ni wazalendo na wamewekeza kwenye michezo na hasa soka.
Mamilioni ya fedha yamewatoka kwa ajili ya kuwekeza, Azam FC leo inaonekana ni bora tofauti na kama unazungumzia matendo, basi yenyewe ndiyo inastahili kuitwa kongwe na si changa tena.
Azam FC imegeuka kuwa presha kubwa kwa Yanga na Simba, lakini nazo zitafurahi kusikia wakati fulani imeharibu jambo fulani.
Hivi karibuni, kiungo Mganda Brian Majegwa alirejea nchini na kuibukia Simba SC. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi akasisitiza bado alikuwa ni mchezaji halali waliyempeleka kwa mkopo KCCA ya kwao Uganda. Sasa vipi aibukie Simba.
Majegwa akasema yuko nchini kwa ombi lake binafsi kufanya mazoezi Simba ili kulinda kiwango chake na alipitia hadi TFF ili kupata ruksa ya hilo.

Lakini katika mahojiano na gazeti maarufu la michezo la CHAMPIONI, Majegwa alisisitiza kuwa Azam FC haikumlipa mshahara wake wa miezi mitatu.
Mganda huyo alilalama kwamba Azam FC ilishindwa kumlipa mshahara huku bibi yake akiwa katika hali mbaya kiafya.
Kauli hiyo ya Majegwa si nzuri kwa Azam FC na hapo ndipo alipoanza kwenda Simba. Sasa amekuwa wazi na anasisitiza anaona bora kuichezea Simba.
Azam FC wamekuwa kimya katika hilo, lakini ili kuendelea kulinda heshima ya klabu hiyo, vema kulitolea ufafanuzi suala hilo.

Mara kadhaa, nimeingia kwenye vijiwe vya mtaani na ajabu wengi wanahoji kama kweli Azam FC inaweza kushindwa kumpa mchezaji mshahara kwa miezi mitatu?
Hii inaonyesha imani ya wapenda soka kwa Azam FC ni kubwa sana. Hivyo wengi wanatamani kusikia uongozi wa Azam FC ukilizunguzmia hili na kuliweka wazi ili kujua tatizo.


Heshima ya Azam FC imepanda haraka sana kwa kuwa imekuwa ikifanya mambo yake kwa mpangilio wa juu. Sasa, hili la Majegwa nalo lipewe kipaumbele ili kuepusha kuitia madoa heshima ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic