November 24, 2015


Na Saleh Ally
Ndoto ya kitu kizuri unachotaka kufanya huanza mapema hasa kama unakuwa umenuia kweli.

Ukitamani kuwa mchezaji, tena maarufu, ikiwezenana nahodha basi ujue inawezekana kwa asilimia nyingi kulingana na wewe unatakaje.
Mwenyezi Mungu ametupa binadamu nafasi kubwa ya kufikia kila tunachokitaka. Mara nyingi ukikosa kitu fulani ujue hukutana au hukuwa na subira wakati unaendelea kupambana kukipata.
Katika picha unayoiona ni kiungo mstaafu wa Barcelona, Xavi Harnandez ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu ya watoto ya Barcelo, nahodha wa timu ya vijana na baadaye ya wakubwa hadi anastaafu na kwenda kucheza soka Uarabuni.
Wakati anakwenda kucheza Qatar, Xavi alikuwa ameshinda kila taji linalotambulika katika ngazi ya klabu.


Amefikia hapo kwa kuwa hakuchoka wala kukata tamaa ya kupambana hadi kupata anachotaka. Wewe umewahi kupambana hivyo, umewahi kuwa na subira huku unajituma au ukikosa leo kesho haurudi? Yote nakuachia mwenyewe lakini juhudi na maarifa ukivichanganya na subira, hakuna linaloshindikana.
Kikubwa zaidi acha maneno mengi kuliko utendaji, acha kulalamika sana huku ukiwa haujafanya lolote kama ilivyo kwa Watanzania wengine. Badala yake pambana, kuwa mtendaji zaidi na kila utakacho, siku ikifika utakipata tu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic