November 25, 2015


Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amegonga hodi kwa kikosi cha Azam FC na kumuomba mshambuliaji wa timu hiyo Kelvin Friday ambaye amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi hicho kwa sasa.


 Mpaka sasa Mwadui bado haijafanikiwa kumsajili mchezaji yeyote ingawa ina mpango wa kusajili wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.

Julio alisema anahitaji kuboresha kikosi chake ndiyo maana ameamua kumchagua mshambuliaji huyo wa Azam.

Julia alisema anahitaji kuwa na kikosi chenye ushindani na kuhakikisha safu yake ya ushambuliaji inakuwa imara.

“Ni kweli namhitaji Kelvin Friday yule wa Azam wakinipatia yule atanifaa sana ndani ya kikosi changu kwa sababu ninahitaji kukiboresha kidogo hasa kwenye safu ya ushambuliaji,” alisema Julio.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic