November 25, 2015


Kiungo mtaratibu aliyewahi kuiliza Yanga mara katika mechi ya Mtani Jembe? Awadhi Juma sasa mkataba wake wa kuichezea Simba unamalizika.


Awadhi alijiunga na timu hiyo msimu wa 2012/13 akitokea Mtibwa Sugar ambaye mkataba wake wa kuendelea kuichezea timu hiyo unamalizika mapema Desemba, mwaka huu.

Kiungo huyo, atakumbukwa kwa kufunga mara zote mbili kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe inayowakutanisha Simba na Yanga mwaka 2013 na 2014.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Muingereza, Dylan Kerr alisema kiungo huyo amemaliza mkataba wa kuichezea Simba, lakini ametoa pendekezo la kuongezewa mkataba mwingine.

Kerr alisema, kiungo huyo ni kati ya viungo bora na kutegemewa kwenye kikosi chake kutokana na uwezo wake wa kuchezesha na kutuliza timu kwa kukaa na mpira na kupiga pasi safi.

 “Kama siyo majukumu ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes, basi Awadhi angekuwa tayari ameongeza mkataba wa kuendelea kubaki kuichezea Simba kwenye vipindi vijavyo.


“Lakini mara baada ya kurejea nchini akitokea Ethiopia kwenye michuano ya Chalenji wanayoshiriki Zanzibar Heroes atasaini mkataba mwingine kwani bado namuhitaji kikosini,” alisema Kerr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic