November 29, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema vijana wana nafasi kubwa katika kikosi chake, kama wataonyesha juhudi.


Pluijm amesema kama kuna vijana wataonyesha juhudi, maana yake wanataka kushirikiana naye kuifanya Yanga kuwa bora zaidi, basi mara moja atawapa nafasi.

"Vijana lazima wakuzwe, lakini vizuri kuangalia mwenye nia ya kutaka kufanya vizuri. Vijana watakaojituma na kuonyesha nia, basi nitawapa nafasi.

"Napenda kukuza vijana, lakini nafurahi nikiona kijana mwenyewe anaonyesha nia ya kutaka kukuzwa na kuendelezwa," alisema Pluijm, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi.

Yanga imekuwa ikifanya maandalizi ya nguvu kujiandaa na Ligi Kuu Bara itakayorejea tena kwenye ratiba Desemba 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic