November 29, 2015



Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Ole Gabriel amewashukuru vijana waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu.
Live Your Goal ni program inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa miguu.
Programu hii iliyomalizika leo imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani Geita.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic