November 28, 2015


Katika harakati ya kujiweka sawa, Simba kesho Jumapili inakwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi huku Kocha Dylan Kerr, akifurahia ushambuliaji pacha wa Danny Lyanga na Hija Ugando.

Mabosi wa Simba wamepiga hesabu na kuona Zanzibar ni mahali pazuri panapofaa kwa kambi yao ya muda kuelekea mechi na Azam ambayo inatajwa kuamua hatma ya Kerr kama atabaki au vinginevyo.

Kerr amesema kuwa: “Tunaenda Zanzibar Jumapili (kesho) kuweka kambi ya siku 10 kabla ya mchezo wetu na Azam, naamini kambi hii itatusaidia kupata kitu tofauti kwani tunacheza na timu nzuri.”

Wakati huohuo, Kerr ameonyesha wazi furaha yake kutokana na uwezo mkubwa ulionyeshwa na mastraika wake Hija Ugando na Danny Lyanga.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Karume, Dar,  Kerr aliwachezesha pamoja washambuliaji hao ambao walionyesha uwelewano mkubwa.

Ugando ambaye yupo majaribio katika kipindi hiki akisubiri majibu ya majaribio kwenye kikosi cha Atalanta ya Ligi Kuu Italia, alionekana kuwa bora zaidi kwa kufunga mabao matatu katika mazoezi hayo huku yote akitengenezewa na Lyanga.

 “Nimefurahishwa nao kwa sababu walikuwa wakicheza kwa kuelewana na wametengeneza nafasi nyingi licha ya kufanikiwa kufunga mabao matatu.


“Nadhani watanisaidia ingawa bado ni mapema kutolea uamuzi kwa sababu yule Ugando bado yupo katika majaribio ila nimefurahishwa na walichokifanya leo,” alisema Kerr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic